Nchi Wanachama Wa SADC Kuimarisha Sera Na Kujenga Mikakati Ya Pamoja Ya Kukuza Ajira Kwa Vijana
Na; Mwandishi Wetu Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimejizatiti kuimarisha Sera na kujenga mipango ya pamoja itakayowezesha kukuza ajira kwa vijana katika Ukanda huo. Akifungua Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa Jumuiya hiyo wanaosimamia Sekta ya Kazi na Ajira hii leo Machi 2, 2020 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alisema kuwa Mkutano huo umewakutanisha Wataalamu wa sekta ya Kazi na Ajira kwa lengo la kuandaa nyaraka mbalimbali zitakazo jadiliwa katika Mkutano wa Mawaziri ambao utafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 5 hadi 6 Machi, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Alieleza kuwa ajenda zitakazo jadiliwa ni pamoja na masuala ya kisera kuhusu ukuzaji wa ajira kwa vijana, pia masuala yanayohusisha uhamaji wa nguvu kazi ndani ya jumuiya ya SADC ambapo it...