Posts

Showing posts from July, 2021

Nchi Wanachama Wa SADC Kuimarisha Sera Na Kujenga Mikakati Ya Pamoja Ya Kukuza Ajira Kwa Vijana

Image
Na; Mwandishi Wetu Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimejizatiti kuimarisha Sera na kujenga mipango ya pamoja itakayowezesha kukuza ajira kwa vijana katika Ukanda huo. Akifungua Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa Jumuiya hiyo wanaosimamia Sekta ya Kazi na Ajira hii leo Machi 2, 2020 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alisema kuwa Mkutano huo umewakutanisha Wataalamu wa sekta ya Kazi na Ajira kwa lengo la kuandaa nyaraka mbalimbali zitakazo jadiliwa katika Mkutano wa Mawaziri ambao utafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 5 hadi 6 Machi, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Alieleza kuwa ajenda zitakazo jadiliwa ni pamoja na masuala ya kisera kuhusu ukuzaji wa ajira kwa vijana, pia masuala yanayohusisha uhamaji wa nguvu kazi ndani ya jumuiya ya SADC ambapo it...

Sekretarieti Ya Ajira Yatakiwa Kutenda Haki Ili Kuiwezesha Serikali Kupata Watumishi Wenye Sifa Stahiki

Image
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kuendelea kutenda haki katika kuratibu mchakato wa ajira ili kuiwezesha Serikali kupata watumishi wenye sifa stahiki na maadili mema ambao watatoa huduma kwa umma kwa kuzingatia weledi na kuwajali wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za umma. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Sekretarieti hiyo na kujiridhisha namna Sekretarieti hiyo inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku. Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kinatakiwa kutenda haki ili Serikali ya Awamu ya Tano ipate watumishi wenye sifa na vig...